Chitika

Sunday, March 9, 2014

Wenger kucheza mchezo wake wa 1000 na Jose Mourinho English Premium League

Wenger v Mourinho

Kati ya michezo ya ligi kuu ya Uingereza isiyopendwa na kocha Arsene Wenger ni dhidi ya Chelsea ya Mourinho. Wakiwa mahasimu wakubwa, Bosi Arsene Wenger anahofu huenda Morinho akaifanya siku yake ikajawa na majonzi.

Saturday, March 8, 2014

UWANJA WA MICHEZO: Arsenal yaelekea Wembley

UWANJA WA MICHEZO: Arsenal yaelekea Wembley

wanadiplomasia wa Kinyarwanda watimuliwa Afrika ya Kusini

Paul Kagame;Rais wa Rwanda

Afrika ya kusini imewaondoa wanadiplomasia watatu raia wa Rwanda ikiwahusisha na shambulizi dhdidi ya makazi ya kiongozi wa zamani wa Rwanda Kayumba Nyamwasa.
Taarifa zinabainisha kuwa Rwanda nayo imeamuru kuondolewa kwa wajumbe sita wa Afrika ya kusini .
Hatua hizo zinakuja baada ya watu wenye silaha kushambulia makazi ya Kayumba Nyamwasa aliyewahi kushika wadhifa wa juu katika serikali ya Rwanda.
Hata hivyo wakati shambulizi hilo mkosoajii wa raisi Kagame Kayumba Nyamwasa hakuwepo nyumbani.
Generali Nyamwasa ameponea chupuchupu majaribio mawili ya kumuua ambapo mnamo mwaka 2010 alipigwa risasi na kujeruhiwa tukio ambalo Rwanda ilikanusha kuhusika

Kwa Habari zaidi Bofya hapa:-                                                                                                       http://mchambuzihotnewz.blogspot.com/2014/03/wanadiplomasia-wa-kinyarwanda.html 

Thursday, March 6, 2014

Jack Wilshere nje wiki sita

Jack Wilshere

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Jack Wilshere atakosa kucheza wiki sita baada ya kupata jeraha la mguu katika mechi aliyochezea England hapo juzi iliposhinda Denmark bao moja kwa bila. Kwa sababu hiyo atakosa mchuano wa FA wa robo fainali hapo kesho dhidi ya Everton na Jumanne ijayo atatazama tu timu yake ikicheza na Bayern Munich katika kombe la kilabu bingwa barani ulaya.
Si hayo tu atakosa mechi nne muhimu za ligii ya England kati ya Chelsea, Manchester City, Swansea na Tottenham ambazo zinacheza mwezi huu.

Obama na Putin wajadiliana kuhusu Ukraine

Rais Obama na Putin

Rais Obama amefanya mazungumzo zaidi ya kina na rais wa Urusi Vladmir Putin akisistiza kuwa vitendo vya nchi yake katika jimbo la Crimea ni ukiukaji wa mipaka na uhuru wa taifa la Ukraine.
Wakati wa mazungumzo yao ya pili kupitia njia ya simu katika kipindi cha siku sita zilizopita, bwana Obama amependekeza njia ya kusuluhisha mzozo huo kidiplomasia inayojumuisha Urusi kuwaondoa wanajeshi wake katika jimbo la Crimea. Bwana Putin amesema uhusiano kati ya Moscow na Washington haufai kutatizika kutokana na mzozo wa Ukraine.
Awali bwana alisema kuwa kura ya maoni iliyopendekezwa kuhusu jimbo la Crimea kujiunga na Moscow inakiuka sheria ya kimataifa na sharti ijumuishe serikali ya Kiev iwapo itaandaliwa.
Akizungumza baada ya mkutano mwingine wa Baraza la Usalama uliofanyika faraghani, balozi wa Uingireza katika umoja wa mataifa , Mark Lyall Grant, amesema haiwezekani muafaka kupatikana katika baraza hilo kuhusu mzozo huo.
"Nadhani hakuna dalili kwamba kutakuwa na mwafaka katika baraza la usalama katika kipindi cha siku chache zijazo. Kama ulivyosikia kutoka kwa wengine, kuna mashauri yanayoendelea kati ya wanadiplomasia kwenye mikutano mbali mbali Ulaya. Mashauri hayo yataendelea,'' amesema bwana Grant.
''Pengine kiwango fulani cha makubaliano kitaafikiwa ili kutuliza mgogoro huu na kisha baraza la usalama pengine litapata suluhu. Lakini hatujafutilia mbali mpango wa kuwasilisha azimio mbele ya Baraza la Usalama wakati wowote na tunafuatilia hali ya mambo kwa karibu tukitarajia baraza la Usalama likutane tena katika siku chache zijazo ikitegemea kitakachotokea mashinani."
Mzozo huo wa Ukraine umechochea wanasiasa pamoja na wageni wengine mashuhuri kususia mashindano ya Olimpiki ya wanariadha walemavu nchini Urusi. Marekani imeondoa ujumbe wake katika michezo hiyo na mawaziri wa Uingereza hawatakuwepo sawia na wenzao kutoka mataifa mengine ya Ulaya.
Habari na BBC SWAHILI

Wednesday, March 5, 2014

Carles Puyol Kutimka Barcelona

Carles Puyol

Nahodha wa klabu ya Barcelona Carles Puyol ametangaza atawahama mabingwa hao wa Hispania mwishoni mwa msimu huu.
Puyol mwenye umri wa miaka 35 aliibukia kutoka vikosi vya vijana wa Barcelona na kujiunga na kikosi kikuu mwaka 1999.
Amewachezea mabingwa watetezi wa La Liga takriban mara 400.
Ameshinda vikombe sita vya ubingwa wa Ligi,vikombe vitatu vya klabu bingwa ya Ulaya,vikombe viwili vya shirikisho la kandanda la Uhispania pamoja na vikombe vya super cup vya klabu za ulaya na Uhispania.
Pia amekua mchezaj muhimu katika nyanja ya kimataifa akiisaidia Hispania kunyakua ubingwa wa bara la Ulaya mwaka 2008 na kombe la dunia miaka miwili badae.
Hata hivyo amekua akisumbuliwa na magoti katika miaka ya hivi karibuni na hakuweza kushiriki katika michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2012.
Msimu huu ameichezea Barcelona mara 12 tu.
Puyol, ambae ameiwakilisha Hispania mara 100,alicheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Uruguay, Februari 2013.
Amesema angependa kupumzika baada ya kuondoka Barcelona. "sijui ntakachofanya baada ya Juni 30 lakini nina hakika nitapumzika" akaongeza.
"nitaitisha mkutano na waandishi habari mwishoni mwa msimu huu ili niwaage baada ya kuichezea klabu hii kwa muda wa miaka 19 ," alisema Puyol

Monday, March 3, 2014

Angalia picha za ajabu: Nyoka apigana na mamba na kummeza


Nyoka ammeza mamba mzimamzima
Chatu akipigana na mamba mwenye urefu wa futi sita kaskazini mwa mlima Isa ulioko Outback Queensland

Hatuwa ya Urusi kuwatuma wanajeshi wake katika mji wa Crimea yazua wasiwasi nchini Ukraine

Malori ya kijeshi ya Urusi katika mji wa Crimea

Waziri Mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk anasema taifa lake liko katika hali ya hatari na ameishtumu Urusi kutangaza vita dhidi ya nchi yake. Wanajeshi wa Urusi kwa sasa wanapiga kambi katika mji wa Crimea ambao upo mpakani mwa mataifa hayo mawili na maakazi ya wananchi wa Mataifa yote mawili.

Mkenya Lupita Nyong'o anyakua tuzo ya Oscar

Lupita Nyong'o

Kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi mwigizaji mashuhuri kutoka Kenya Lupita Nyong'o amenyakuwa tuzo la Oscar la mwigizaji msaidizi wa kike kwa jukumu lake la kuelezea masaibu ya Patseh katika filamu ya utumwa ya ''12 Years A Slave.''

Tuesday, February 25, 2014

Boko Haram Wauwa Wanafunzi Nigeria

Boko Haram

Wanamgambo wa Kiislam wa kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria wametuhumiwa kushambulia shule moja na kuwaua wanafunzi kadhaa.